BENKI YA NAFAKA YA JAMII
Utangulizi
Maelezo haya mafupi ya kiufundi yanayotuwasilishia hatua za kuanda na kuendesha benki ya nafaka. Yamejikita katika mfano halisi wa Nthunguni Community Cereal Bank ya wilaya ya Makueni, Kenya. Ni nini Benki ya Nafaka? Benki ya nafaka ni taasisi ya jamii inyohusisha jamii au vikundi vya vijiji ambayo hujiwekea na kusimamia shughuli za kujipatia, kupanga bei na kusambaza nafaka. Nia hasa ya kuwa na benki ya nafaka ni kuboresha usambazaji wa vyakula wakati wa njaa, hasa katika vipindi virefu vya ukame. Jamii husika itaamua aina ya benki ya nafaka itakayoweza kutatua matatizo yao. Nafaka inanunuliwa aidha kutoka kijijini ama kwingineko wakati bei zikiwa nafuu, mara baada ya kuvunwa, inahifadhiwa hadi inapohitajika na kuuzwa kwa bei ya kuridhisha. Kila mmoja hufaidka. Wanavijiji wanalipwa bei bora kwa nafaka yao, wakati bei za masoko zikiwa dumi, jambo linlowawezesha huwa na pesa za kulipa kodi zao, karo ya shule gharama nyinginezo. Wakati bei za nafaka sokoni zikiwa juu na maghala yakiwa tupu, wanaweza kununua nafaka kutoka benki ya nafaka kwa bei nafuu watakayoimudu na kuisafirisha hadi makwao. Hivyo wanaokoa muda na gharama za usafiri.
Picha 1: Mwende Musau mwenye umri wa miaka 11, akiketi karibu na benki ya nafaka akibeba mawele. Picha: Practical Action / Zul.
Kuanzisha benki ya nafaka Hakuna kanuni maalumu za kufuatwa wakati benki ya nafaka inapoanzishwa. Hata hivyo, kunazo hatua za kimsingi za kufuatwa. Kufanya uamuzi Maamuzi ya kuanzisha benki ya nafaka sharti yafanywe kuambatana na mhitji na kila mwanakijiji kama vile uhaba wa nafaka kufuatia ukame wa muda mrefu. Maadamu stoo yenyewe itamilikiwa na kijiji chote, ni muhimu kuwa na mshauriano ya watu wa tabak zote kijijini juu ya: • Aina ya stoo wanayohitaji • Mahali pa kunjenga stoo hiyo • Kupata nafaka ya kuanzia benki hiyo Mikutano kadhaa kijijini ya kupata maafikiano ni muhimu kutegemeana na ukubwa wa kijiji chenyewe. Stoo yenyewe Stoo, ghala au bohari yafaa kujengwa mahali mbapo paweza kufikwa kwa urahisi na kila mtu. Pawe ni mahali salama na panapoweza kulindwa kwa urahisi. Kijiji kizima kiamue mahali itakapojengwa. Sharti kijiji kijadili kwa kina kuhusu vitu vya kujengea ghala hiyo. Waamue kama wanataka stoo ya kudumu au ya muda, ya kuazimwa au ya kukodishwa.
Practical Action, The Schumacher Centre for Technology and Development, Bourton on Dunsmore, Rugby, Warwickshire, CV23 9QZ, UK T +44 (0)1926 634400 | F +44 (0)1926 634401 | E infoserv@practicalaction.org.uk | W www.practicalaction.org ______________________________________________________________________________________________ Practical Action is a registered charity and company limited by guarantee. Company Reg. No. 871954, England | Reg. Charity No.247257 | VAT No. 880 9924 76 | Patron HRH The Prince of Wales, KG, KT, GCB
Banki ya nafaka ya jamii
Practical Action
Kuanzisha benki Kuna njia tatu za kujipatia benki ya nafaka ya jamii; mkopo, zawadi (au msada wa chakula) au usaidizi kutok kw wanajamii, njia hizi tatu zawez kuchanganywa na kurahisisha kazi yao. Mikopo Mikopo yaweza kuwa ya aidha pesa au nafaka, na nyakati nyingine mseto wa vyote viwili. Mkopo wa pesa ndio uliozoeleka saana na huja na masharti ya wastani (K.M. miaka 5) ikiwa na riba au bila riba, au wa muda mfupi (wa mwaka au hata miezi michache) na riba au bila riba. Ni muhimu kwa wana kijiji kuelewa masharti ya mkopo waliopewa. Zawadi Mara nyingine zawadi hasa yaweza kutolewa na shirika la kutoka nje. Hii huwa ni hazina ya kuendesha shughuli za benki hadi mwaka utakaofuata. Pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya nafaka mwaka wa kwanza hutumuka kununulia akiba ya mwaka utakaofuata na endapo mambo yatawaendea vyema katika benki yao, basi misaada kutoka nje huwa hihitajiki. Mchango wa kijamii Jamii yote yaweza kuchangia kwa kulima shamba pamoja na wanaapovuna na kuuza mazao yao kasha pesa zikawekwa katika benki yao ya nafaka. Ama kila mwanakijiji anaweza kutoa mchango wa nafaka baada ya uvunaji na inawekwa katika benki hiyo ya nafaka. Kuchangisha pesa Katika maeneo yaliyo na nafaka ya ziada au kiasi kamili kunachohitajika na wanakijiji, ni muhimu kuanzisha benki hiyo kwa kutumia pesa. Hii itawezesha benki kuwalipa wakulima bei mzuri kwa nafaka zao na pia benki hiyo inayofursa ya kujinunulia nafaka yake yote kutoka kwa wanakijiji wa eneo linaloizunguka.
Mambo ya kufikiriwa stoo inapochaguliwa Stoo ya muda yaweza kujengwa na wanakijiji wenyewe; vitu vya kujengea vyaweza kupatikana humo humo kijijini na itakuwa rahisi kujenga. Lakini haitakuwa imara na itahitaji ukarabati wa mara kwa mara. Uharibifu wa nafaka katika ghala ya kudumu kwa sababu ya muda haina ulinzi wa kutosha dhidi ya wadudu waharibifu. Kwa upande mwingine stooya kudumu (iliyotengenezw kwa matofali na simenti) yaweza kudumu sana ingawa ni ghali kujenga; uharibifu wa nafaka kwa wadudu ni mdogo kwake. Kuanzima ama kukodisha stoo kwaweza kuwa rahisi kuliko kujenga lakini mwenyewe awez kulihitaaji jengo lake ghafla na kusababisha hasara au shida nyingi.
Kuliko na nafaka ya kutosha kwa wanavijiji, kuanzisha benki ya nafaka kwa pesa kutawawezesha wakulima kujipatia bei nzuri kuliko ile ya wafanyi biashara wengine. Lakini sharti benki iongeze juhudi ya kupata nafaka na kuwa tayari kugharimia usafirishaji wake. Hii inawezekana, ingawa sharti viongozi wawe na maarifa ya kutosha juu ya bei wanunue kwa wakati ufaao na mahali mwafaka. Kwa kutumia pesa kutailazimu kamati ya usimamizi wa benki kukabiliana na hali halisi ya soko la nafaka na ushindani wa wafanyibiashara kutoka mwanzoni. Kamati hiyo pia itajifunza namna ya kuendeleza shughuli za benki rasmi kwani itafungua akaunti katika benki ya biashara katika mji wa karibu, isimamie akaunti za wanachama wa benki hiyo ya nafaka na kuweka za faida. Haya yote yaonekana kuwa mambo yatoshayo kuanzisha benki ya nafaka. Ipo hatari kwamba kijiji chaweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa kuifadhili benki yao na kushawishika kuzitumia katika miradi yao mingine. Kuanzisha kwa akiba ya nafaka Faida kubwa ya kuanzisha akiba ya nafaka ni kwamba vijiji, hasa vile visivyozalisha nafaka ya kutosha, kwa jumla ni rahisi kujitimizia mahitajo yao yote ya chakula. Iwapo kamati ya usimamizi utajishughilisha na nafaka pekee, hawatajua jinsi ya kusimamia pesa na pia soko la nafaka linavyoendesha mambo yake. 2
Banki ya nafaka ya jamii
Practical Action
Ipo pia hatari ya kijiji kuiona benki yao ya nafaka kama msaada tu wa chakula. Hivyo, ni vyema kuianzisha benki hiyo kwa nafaka pamoja na pesa. Muundo wa benki ya nafaka Wanachama wa benki ya nafaka ndio wanaoilmiliki benki. Mtu yeyote katika jamii ambaye analithamini wazo la kuwa na benki ya nafaka na ambaye atafaidika nayo ni mwanachama wa benki hiyo. Wanachama wa benki hiyo wataamua lengo la kuwa na benki hiyo na pia watakavyoiendesha kwa mfano, iwapo itakuwepo kuhudumia matakwa ya jamii pekee, ama ni ya kuwaletea faida), na watasimamia shughuli zote za benki hiyo wanachama wa benki hiyo ya nafaka kwa kawaida hukutana mwanzini mwa kila msimu.
Kamati ya usimamizi wa Benki ya Nafaka Wanachama wa benki ya nafaka huchagua kamati ya usimamizi ambayo huwa na mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mtu wa kusimamia stoo na wanunuzi. Kwaweza kuwa na makaimu katika nyadhifa kadhaa watakaofanya kazi nyakati za ugonjwa wa wanakamati Fulani. Kamati ya usimamizi huwajibika katika mambo manne makuu: • Kusimamia shughuli za kila siku za benki hiyo ya nafaka. • Kupendekeza kwa wanachama sera mwafaka za biashara na pia ushirikiano wa kijamii. • Kukagua shughuli za benki za kila mwaka. • Kujibu maswali ya wanachama kuhusu benki yao.
Mambo yanayoweza kwenda mrama • Kamati ya usimamizi wa benki hiyo ya nafaka huenda ikakosa wanakamati wenye ujuzi muhimu. • Wanachama wa benki ya nawaka wanahitaji kuelewa jinsi beni kiyo inavyoendesha mambo yake. Endapo watashindwa kuelewa basi hawatalipa madeni yao. • Katika maeneo ambapo nafaka haikuzwi, inaweza kuwa shida kwa benki kupata nafaka ya kutosha ya kununua. • Hazina ya kuendesha yaweza kuwa ndogo sana kununulia nafaka ya benki hiyo ili kuiwezesha kuendelea. • Kama pesa zinazopokelewa kutoka kwa mashirika ya nje zitafika zikiwa zimechelewa sana, benki haitaweza kununua nafaka bei zitakaposhuka. • Kukosa uaminifu kwa kamati ya usimamizi.
Kazi ya mwenyekiti ni kusimamia shughuli za benki. Yenye huwa ndiye nguzo muhimu ya mawasiliano na watu wa nje. Naye katibu kazi yake ni kuandika rekodi za shughuli zote za utawala na hesabu za benki nafaka. Mtunza stoo huingiza ndani nafka inayonunuliowa na kasha kuiuza. Huitunza stoo hiyo na hali ya nafaka iliyomo ndani. Mweka hazina hutunza pesa. Wanunuzi hupanga ununuzi wa nafaka kwa benki wakati ambapo bei ni nzuri, wakati mwingine wakisafiri masafa marefu na kupanga usafiri wa nafaka hadi kijijini. Sifa za kamati ya usimamizi ufanisi wa benki ya nafaka Ufanisi wake hutegemea uhodari na uwajibikaji wa kamati ya usimamizi. Hivyo, kamati hiyo sharti iwe na watu waaminifu, waadilifu, wenye uwezo mkuu, waliosoma na kujitolea kwa maslahi ya kijiji. Wanachama wa benki ya nafaka wa benki ya nafaka sharti wachague kamati hiyo kwa makini sana na baadhi ya kazi zitahitaji sifa maalumu kuliko nyingine. Kwa mfano, mwenyekiti sharti awe mtu wa kusikiza wengine, anayeweza kuunganisha watu na hodari wa kushauriana. Katibu lazima awe mtu aliyesoma na anayejua kufanya hesabu. Ni rahisi kuju mahitaji kadhaa kama kujua kusoma lakini sivyo kwa wengine kama uaminifu na kujitolea. Kamati ya usimamizi wa benki ya nafaka sharti iwe na wanawake na wanaume wa tabaka zote, idara zote na pia kila umri. Sharti kamati hiyo iwe na watu wa aina zote na wala siyo kutawaliwa na watu wa kundi Fulani au mtu binafsi. Mafunzo ya kuongeza maarifa 3
Banki ya nafaka ya jamii
Practical Action
Baadhi ya kazi za kamati ya usimamizi huhitaji maarifa au stadi maalum. Kwa mfano mwekahazina lazima ajue stadi za kimsingi za uhasibu ili amudu kusimamia vitabu hivyo. Utaratibu huo huhusisha uhifadhi wa kitabu cha mweka hazina, afisa wa ununuzi na mtunza stoo lazima wafunzwe taratibu za uhasibu. Afisa wa ununuzi pia anahitaji kufunzwa stadi bora za ununuzi. Iwapo wanachama wa benki hawatapata watu wenye sifa na maarifa hayo, sharti watafute watu wenye sifa tofauti na walio radhi kusoma. Inawezekana kumpata mtu kutoka nje ambaye anaweza kuifunza kamati ya usimamizi baadhi ya shughuli hizi. Uendeshaji wa benki ya nafaka Ni jukumu la benki kuamua kiasi cha nafaka itakayowasheleza wanakijiji katika msimu wa njaa. Hii ni muhimu kabla ya kuanza shughuli nyingine zozote. Benki hushughulika ununuzi wana uuzaji kuitumia kuwasaidia walio na shida. Kununua nafaka Benki ya nafaka hununua nafaka mara tu baada ya uvunaji. Wakati bei zikiwa chini. Itanunua kwanza kutoka kwa wanachama wake, halafu vijiji vya karibu, kwa wafanyibiashara na kisha kutoka kwa benki nyingine za nafaka za karibu. Bei wanayonunulia nafaka kutoka kwa wanachama wake na vijiji vya karibu yaweza kuwa ya juu kuliko ile ya sokoni. Lakini wanaponunua kutoka kwa wafanyibiashara hawafai kulipa zaidi ya bei za sokoni. Kuuza nafaka Wanachama wa benki ya nafaka wataamua watakapoanza kuuza nafaka ya wataamua iwapo wataiuza mwaka wote au msimu wa njaa tu. Mara nyingi, uuzaji hufanyika wakati wa njaa ambapo watu wengi huwa wameishiwa na chakula na ni ghali kukinunua sokoni. Ingawa hivyo, itategemea sana yale wanayotaka wanachama wa benki hiyo. Hii ni kawaida hasa katika maeneo ambayo hayazalishi chakula cha kutosha na za wafugaji ambazo kabisa hazishiriki katika kilimo. Hata hivyo, uuzaji wa wakati wote wa mwaka hutaka kamati nzuri ya usimamizi. Mara nyingi benki ya nafaka haitaki kuuza bidhaa ya hadi bei zinapokuwa juu kabisa katika soko huru. Huu ni uamuzi unaokuwa umefanywa na wanachama wa benki hiyo. Kwanza, benki huwauzia wanachama wake nafaka hiyo. Kama itakuwepo ya ziada basi itauzwa kwa wasio wanachama. Wanachama hulipa bei ya chini kuliko ya wasio wanachama. Sharti bei ya kuuzia ipangwe kulingana na gharama ya kununulia iliyotumiwa mapema. Lazima iwe chini kidogo ya ile ya sokoni katika vijiji jirani, lakini sharti iwe sawa au juu kidogo ya bei ya kununulia. Pia ni muhimu kwa benki kuuza nafaka kwa kiasi kidogo ama kikubwa kwani si wote walio na uwezo wa kununua kiasi kikubwa kila mara. Kuwasaidia wasiojiweza kabisa Kunapokuwa na uhaba wa chakula kila mtu huwa anataka kununua nafaka kutoka benki na maadamu si wote wenye uwezo sawa, matajiri huenda wakanunua nafaka yote na kuwaacha wengine bila chakula. Kutokana a hili, benki ya nafaka lazima iwe na msimamo kamili kuhusu sera yake na iwe na mfumo wa kudhibiti ununuzi na uuzaji, ama sivyo wasojiweza kiuchumi hawatafaidika kutokana na kuweko kwa benki hiyo. Benki ya nafaka ina njia nyingi za kuwasaidia maskini. Hizi ni baadhi ya njia hizo: Kupanga migao Hii ina maana kwamba benki hiyo inachunguza kiasi cha nafaka kilichomo ndiposa inaruhusu kila mwanachama kiasi Fulani. Badala yake pia, benki yenyewe inaamua kiasi cha nafaka kinachohitajika na familia. Kwa mfano, benki ya nafaka yaweza kuamu kwamba kila kiongozi katika familia anunue kila 100 kila baada ya siku 15. Hii itazuia watu binafsi kununua kiasi kikubwa na kidogo cha nafaka kutoka katika benki yaweza kuruhusu watu kununua nfaka katika benki hiyo watakapo na kulingan na kiasi cha pesa wlichoncho. Mkopo 4
Banki ya nafaka ya jamii
Practical Action
Wanachama wa benki ya nafaka wanaweza kuruhusu watu kununua nafaka kwa mkopo. Lakini ikifanya hivyo, sharti iamue: • Ni watu wangapi ambao waweza kuhitaji mkopo? • Ni kiasi gani cha nafaka kilicho stoo ambacho benki yaweza kuuza kwa mkopo? • Ni kwa vipi benki itakabiliana na wale ambao hawatalipa madeni yao? Hazina ya jamii Benki ya jamii inaweza kuanzisha hazina ya jamii. Kwa mfano, benki inaweza kumfanya kila mtu anayenunua nafaka kutoka katika benki hiyo kutoa mchango mdogo utakaoingia katika hazina hiyo ya jamii kuwasidia maskini katika jamii.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Eric Kisiangani, Practical Action – East Africa Box 39493 - 00623 Nairobi Kenya Tel: +254 2 719313 Fax: +254 2 710083 E-mail: erickisiangani@itdg.or.ke Practical Action The Schumacher Centre for Technology and Development Bourton-on-Dunsmore Rugby, Warwickshire, CV23 9QZ United Kingdom Tel: +44 (0)1926 634400 Fax: +44 (0)1926 634401 E-mail: inforserv@practicalaction.org.uk Website: http://practicalaction.org/practicalanswers/
Practical Action is a development charity with a difference. We know the simplest ideas can have the most profound, life-changing effect on poor people across the world. For over 40 years, we have been working closely with some of the world’s poorest people - using simple technology to fight poverty and transform their lives for the better. We currently work in 15 countries in Africa, South Asia and Latin America.
5
Post a Comment